Mwongozo Wa Biashara Ya Mtandao Ya Kampuni Ya Green World Kwa Afrika Mashariki

Namna Ya Kufanya Presentations

kuandaa presentation


Kufanya presentations zenye mafanikio ni kitu muhimu katika kukuza na kuendeleza biashara yako mpya ya Green World. Mtu anapoonyesha nia ya kujifunza zaidi juu ya fursa ya biashara ya Green World, unaweza kufanya moja ya presentations zifuatazo:

Presentation Ya Kundi

Ukiona kuna haja ya kufanya mkutano na watarajiwa, fanya hivyo mara moja. Kama kuna haja ya msaada wa usafiri usisite kutoa lifti na kuongozana nao. Tumia mbinu zako zote za kibiashara; fika kwa wakati, zingatia utanashati, onyesha matumaini, kuwa msikivu na usifanye vitu kwa kulazimisha. Ni busara kwenda kwa mtarajiwa "almasi" na kuachana na yule ambaye haonyeshi kuvutiwa na fursa aliyopewa.

Lazima utegemee kuwa ni asilimia 40 hadi 50 tu ya watu walioahidi kuhudhuria ndio watakaofika. Ni jambo la kawaida kabisa, usikatishwe tamaa bali endelea kupanga mipango yako ya baadaye. Kama unalenga wanandoa wawili kuhudhuria mkutano wako, basi alika 10. Uwiano huu utazidi kuwa mzuri kadri utakavyoboresha mbinu zako za ufuatiliaji.


Kuchagua Na Kuandaa Chumba Cha Mkutano


Kama utafanya presentation ya kundi wewe mwenyewe, unaweza kuchagua kuifanya nyumbani kwako au kwenye ukumbi wa nje kama kwenye hoteli au jumba la jumuia. Unapochagua ukumbi wa mkutano, zingatia yafuatayo:

Weka viti vya kutosha kwa watu unaowategemea tu. Andaa viti pembeni kwa wale watakaochelewa au watakaofika bila kutegemewa.

Presentation Ya Mtu Mmoja

Unaweza kuona kuwa utapata matokeo mazuri zaidi kwa kumwelezea mtu kuhusu fursa ya Green World kwenye mazingira rahisi na yasiyo ya rasmi kwa kufanya presentation ya mtu mmoja. Mpe maelezo ya bidhaa na fursa ya biashara kwanza. Mpe maelezo ya thamani na faida za fursa hii. Baada ya kuiangalia video kwa pamoja, mpe nafasi ya kukuuliza maswali. Hii itakupa nafasi ya kugundua ni kitu gani kinachomvutia ndani ya Green World. Elekeza presentation yako upande ule unaomvutia. Jaribu kufanya kila kitu kiwe rahisi. Presentation fupi iliyosheheni hoja ni bora kuliko ndefu ya kuzungukazunguka hata kama hii ya pili ina mvuto kiasi gani.


Kukabiliana Vikwazo Kwenye Presentaion Ya Mtu Mmoja


Kama mtarajiwa wako anauliza maswali au anatoa vikwazo, hii ni ishara nzuri. Tumia nafasi hiyo kutia mkazo kwenye imani yako juu ya thamani ya bidhaa za Green World. Mtarajiwa akishaanza kuuliza maswali, unayo nafasi ya kujenga urafiki. Kumbuka kuwa vikwazo vinavyotolewa ni namna nyingine tu ya maswali ambayo yanahitaji majibu au ni namna ya kutaka kuondolewa hofu na hali ya kutojiamini. Kutoa majibu mazuri kuhusu vikwazo vyake kunaweza kusababisha mafanikio makubwa kwenu wote wawili.


kuandaa presentation


Kwa mfano, mtarajiwa akisema kuwa hataweza kuuza bidhaa, kwa maana nyingine ni kuwa anataka umhakikishie kama kweli ataweza kuuza hizo bidhaa. Mhakikishie kuwa atauza tu! Mwambie pia kuwa wewe msajili wake na kikosi kizima cha Green World kitakuwa karibu yake kumpa msaada ... kumfundisha namna ya kuuza bidhaa! Kumbuka, wewe ukionyesha ari na kuwaeleza watarajiwa wako jinsi unavyojisikia kuhusu Green World ..... mengine yatajipa yenyewe.


Kufanya Presentation


Anza kwa wakati uliopangwa. Wageni wako wanathamini muda na watafurahi kuona kuwa pia unathamini muda.

Usiruhusu presentation yako kuchukua zaidi ya dakika 45. Presentation fupi, ya kimuhtasari itakuwa na matokeo mazuri zaidi ya ile ndefu ya kuzungukazunguka. Msalimu kila mmoja wa wageni wako. Matumizi ya vitambulisho kwa kila mtu huwa ni bora.


Kutumia Video


Video ya Green World inasisimua na ni njia inayotoa mafanikio mazuri sana katika kumpa mtarajiwa picha ya jumla ya fursa ya kampuni.

Upatikanaji: Video ya Green World inaweza kutumika kirahisi na watarajiwa wengi.

Msaada: Video ya Green World imeandaliwa kumsaidia hata mgeni kwenye kampuni hii kuweza kutoa presentation. Inasaidia kuondoa hofu ambayo watu wengi hupata wanapokabiliwa na kutoa presentation.

Uwanja Mpana: Video hii imeandaliwa kuweza kutumika kwenye kila aina ya mazingira ya kutangaza biashara - rasmi na yasiyo rasmi.

Kusajili: Video ya Green World ni kifaa bora katika kusajili watarajiwa. Yafaa kila wakati kuwa na nakala chache za video hii. Unapomwazima mtarajiwa mwambie kuwa unapenda aiangalie video hii kisha akuambie anafikiria nini kuhusu alichokiona. Ufuatiliaji ni muhimu. Panga muda wa kwenda kuichukua video hiyo.

Mwendelezo: Kama kila mmoja wa wafuasi wako katika jumuia yako atatoa presentation kamilifu kama ulivyofanya wewe, kwa hakika kutakuwa na mwendelezo wa juhudi zako. Video imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu. Video hii si tu inakusaidia kuendeleza juhudi zako kwa kuwafikia watu wengi zaidi bali inahakikisha kuwa watu ndani ya jumuia yako ya biashara wanapata mafunzo kwa kutumia taarifa ambazo zimepasishwa na kutolewa na kampuni ya Green World.

Zingatia kuwa video hii ipo pale kukusaidia katika shughuli zako na si kuchukua nafasi yako. Wewe pekee ndiye unayeweza kuamsha ari ya watarajiwa kuhusu fursa ya Green World. Ni wewe pekee ndiye unayeweza kutoa ushahidi wa matokeo ya fursa hii. Ni wewe (ukishirikiana na mwanachama aliyekusajili) ndio mnaoweza kujibu maswali kutoka kwa watarajiwa binafsi na kusajili wanachama wapya - SI MWINGINE, NI WEWE!


Kukabiliana Na Vikwazo Kwenye Presentation Ya Kundi


presentation ya kundi


Kumbuka kuwa vikwazo ni namna nyingine tu ya kuuliza maswali. Kwenye presentation ya kundi ni vizuri kuwaomba wageni kuhifadhi maswali yao hadi mwisho wa presentation. Hii itakusaidia kufuata mpangilio wa presentation yako na kumaliza kwa muda muafaka. Mwishoni, ni wazo zuri kujibu swali moja baada ya jingine. Jaribu kujibu maswali ukiyapa maswali yote umuhimu uliolingana.


Kufunga Mkutano


Unapokuwa tayari kuufunga mkutano, waombe wageni wako kuzungumza na wanachama waliowaalika. Waruhusu wageni hao kuwauuliza maswali. Unakuwa umegeuza presentation ya kundi kuwa presentations za mtu mmoja mmoja na kuruusu wageni kufuata taratibu zinazotakiwa katika kujisajili kama wanachama wa Green World.

Kama ulikuwa unahudhuria presentation ya mtu mwingine ukiwa na mgeni wako, kazi yako ni kuonyesha mapenzi ya biashara yako na kutoa msaada wakati presentation ikiendelea.

Ukiwa umefanya hivyo, tumia mwamko na msisimko walioupata wageni wako kwa kufanya usajili na/au kuuza bidhaa za Green World.


Uhakiki Wa Nyenzo Kabla Presentation.



Vitu Vya Kuzingatia






<<<< MWANZO